Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto bungeni: Mtuhumiwa Zandile Mafe akana mashtaka

Moto Sauziiii Mtuhumiwa Zandile Mafe akana mashtaka

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kesi dhidi ya mwanamume mwenye umri wa miaka 49 anayeshtakiwa kuhusiana na moto kwenye Bunge imeahirishwa hadi Januari 11.

Moto ulizuka katika bunge hilo siku ya Jumapili usiku. Bunge nchini humo lilithibitisha kuwa kumekuwa na “uharibifu mkubwa” katika upande wa jengo jipya la Bunge hilo.

Lilisema upande ulioathirika zaidi unajumuisha ukumbi wa Bunge la Kitaifa ambapo wabunge huketi. Pia ilisema baadhi ya ofisi “zimeharibiwa vibaya”.

Zandile Mafe alifikishwa katika Mahakama ya Cape Town jana asubuhi, akiwakilishwa na Luvuyo Godla.

Mafe alikana mashtaka hayo. Akizungumzia suala hilo, wakili wake, Godla alisema mteja wake amekana mashtaka.

Hakimu Zamekile Mbalo aliahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo ili kutoa nafasi kwa uchunguzi zaidi.

Advertisement Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka katika Rasi ya Magharibi, Eric Ntabazalila alisema wapelelezi wa Serikali walihitaji kuthibitisha habari fulani, kama vile anwani ya makazi ya mshukiwa na kama ana mali.

“Wachunguzi hawajaweza kwenda Bungeni kutathmini uharibifu. Kufikia Jumanne ijayo tutakuwa na taarifa hizo,” Ntabazalila alisema na kuongeza kuwa ingawa mshtakiwa ana haki ya kupata dhamana, lakini Serikali itapinga dhamana.

Mtuhumiwa huyo aliyekamatwa na polisi kabla ya kufikishwa mahakamani hapo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya uvunjaji wa nyumba, wizi na uchomaji moto.

Tangu Jumapili, moto umekuwa ukiteketeza eneo la bunge na kuharibu jengo la Bunge na sehemu za jengo la Bunge la Kale.

Jumatatu alasiri pepo kali za kusini-mashariki katika jiji zilichochea moto tena ambao ulidhibitiwa karibu na usiku wa manane.

Msemaji wa Bunge, Moloto Mothapo alisema, “Baada ya moto kuibuka kwa mara ya pili tulilazimika sasa kupeleka vyombo vya kuzima moto vya angani, ilionekana kabisa vile vilivyotumika awali vimezidiwa.

“Wazima moto walitumia roho ya ushujaa na ujasiri wa mapigano katika mapigano yao kwa saa kadhaa jana usiku, na hadi usiku wa manane walifanikiwa kuzima moto huo.

Mothapo alisema uharibifu zaidi umetokea, huku ofisi za wabunge zikiwa zimeteketea kabisa.

“Pamoja na moto huo sasa timu ya wahandisi wa fani mbalimbali iliyofika bungeni jana inaingia kazini kufanya tathmini na kujua ukubwa wa uharibifu.

“Maofisa wasimamizi wa Bunge wameipongeza timu ya wazima moto kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa siku kadhaa bila kuchoka hata katika mazingira hatarishi, kudhibiti moto,” Mothapo aliongeza.

“Halikuwa jambo rahisi kwa sababu kulikuwa na upepo unaouchochea kuongeza makali,” alisema.

Jengo hilo ni hifadhi kwa maelfu ya hazina mbalimbali za kitaifa, vikiwemo vitabu vya kihistoria, picha na kazi muhimu za sanaa ambazo maofisa walisema zimehifadhiwa.

Taarifa kutoka kwa baraza la jiji ilisema kwamba ghorofa ya nne na ya tano ya jengo hilo ilikuwa imeharibiwa kabisa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz