Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto Wateketeza Gereza, Wafungwa Wahofiwa Kufariki

MOTO 2 Moto Wateketeza Gereza, Wafungwa Wahofiwa Kufariki

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAFUNGWA kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya Gereza Kuu la Gitega nchini Burundi, kuteketea kwa moto Jumanne ya Desemba 7, 2021 majira ya asubuhi.

Picha zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao zinaonesha maiti za watu kadhaa waliofariki dunia kwa kuungua na moto, wanaodhaniwa kuwa wafungwa.

Mamlaka nchini Burundi bado hazijatoa maelezo kuhusu tukio hilo la moto huku mwandishi mmoja wa habari wa shirika binafsi aliyeshuhudia tukio hilo, akinukuliwa na vyombo vya habari akieleza kuwa sehemu kubwa ya gereza hilo imeteketea.

Mfungwa mmoja aliyenusurika ameliambia Shirika la Habari la BBC kuwa moto huo ulizuka majira ya saa kumi alfajiri katika vyumba vya kulala wafungwa ambapo mpaka sasa bado haijafahamika nini kilichosababisha moto huo.

Mwishoni mwa Agosti, mwaka huu kulitokea tukio lingine la moto katika Gereza la Gitega uliosababishwa na hitilafu ya umeme lakini hakukuwa na vifo wala majeruhi kwa wafungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live