Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moses Kuria atofautiana na DP Ruto, asema ni lazima aunde chama chake

1474eecb55b4d600 Moses Kuria atofautiana na DP Ruto, asema ni lazima aunde chama chake

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kuria alisema yuko radhi kumaliza urafiki wake wa kisiasa na vigogo ambao wanapinga kuundwa kwa chama cha Mt KenyaAlisema eneo hilo liko kwenye hatari ya kukosa nafasi ya kutetea maslahi yake baada ya 2002DP Ruto amekuwa akipinga kuundwa kwa vyama vya maeneo akisema hilo litaendeleza ukabilaMbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amesema ni lazima eneo la Mt Kenya liwe na chama chake kwenye siasa za uchaguzi mkuu ujao.

Kuria alisema eneo la Mt Kenya lisipofanya hivyo litabaki shabiki kwenye mchuano wa 2022 wakati Rais Uhuru Kenyatta atakuwa akiondoka.

Kulingana na Kuria, eneo la Mt Kenya halitakuwa na mgombea na hivyo huenda maslahi yake yakakosa kuangaziwa.

Alipuuza Naibu Rais William Ruto ambaye amekuwa akipinga vyama vya maeneo akivitaja kuwa vya kikabila.

"Kama hatutajipanga, sisi Mt Kenya tutakuwa mashabiki tu kwenye mchuanoujao. Na hatufai kuitwa wakabila tukisema tunahitaji vyama vya kila eneo. Hilo ni lazima," alisema Kuria.

Read also

Magazeti Ijumaa Julai 6: DP Ruto Asema Atachomoka Kutoka Serikali Wakati Ukifika

Alimwambia DP kuwa wamekubali kumuunga mkono na hivyo awape nafasi ya kuunda vyama vyao.



"Tumekubali kuwa hatutakuwa na mgombea wa urais kwa mara ya kwanza katika miaka 30. Alafu tena utuambia kuwa hatuwezi kuwa na chama chetu? Hilo haliwezekani, na siogopi kutuwa nje ya serikali ya sasa ama ile ijayo," alisema Kuria.

Kuria alisema itakuwa vigumu kwa maslahi ya maeneo kuwasilishwa serikali bila ya vyama tanzu kwenye serikali hiyo.

"Vyama ndivyo nguzo ya uongozi. Kuna masuala ambayo ni lazima yapiganiwe na vyama vya eneo fulani," alisema Kuria.

"Hatubanduki, kwa hivyo tuzoeane mapema jamaa," Kuria aliongeza akisema kama hilo litaathiri uhusiano wake na DP hatajutia.

Kuria alizua maswali kisiasa baada ya kukosa kuhudhuria mkutano wa UDA nyumbani kwa DP Karen Alhamisi Agosti 5 ambapo wandani wa DP walikongamana.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke