Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moses Kuria amtaka Raila kujiondoa kwenye handisheki, asema imempaka tope

Bcd451572556f5e7 Moses Kuria amtaka Raila kujiondoa kwenye handisheki, asema imempaka tope

Sun, 16 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kuria aliashiria Rais Uhuru anaongoza nchi kwa njia za kiimla na kumtaka Raila kutojihusisha na uongozi huo

- Alisema amekuwa mwanademokrasia kwa miaka mingi na hafai kuharibu sifa hiyo kwa kujihusisha na handisheki

- Raila amekuwa akionekana kuwa mnyamavu kwa maovu ya serikali tangu aingie kwenye mkataba wa handisheki na Rais

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amemtaka kinara wa ODM Raila Odinga kujiondoa kwenye mkataba wake na Rais Uhuru Kenyatta wa handisheki.

Kuria alisema nchi kwa sasa inaongozwa kwa njia ya kifua na kutaka Raila kutojihusisha na yanayoshuhudiwa.

Kwa mjibu wa ujumbe wake kwenye Facebook, mbunge huyo alisema kiongozi huyo wa upinzani anajulikani kwa kupigania demokrasia na wala si uongozi wa kiimla.

Matamshi ya Kuria yaliashiria Rais Uhuru Kenyatta amegeuka dikteta anayewakandamiza wanaomkosoa.

"Kwa Raila Odinga. Wewe haufai kuwa katika upande wa madikteta. Unafaa kuwa mwanademokrasia. Rudi nyumbani Baba. Rudisha sura yako. Wanakufanya ukae mtu mbaya," alisema Kuria.

Wandani wa Naibu Rais William Ruto wamekuwa wakidai Rais amegeuka na kuwa dikteta ambaye anawahangaisha wote wanaoenda kinyume cha matakwa yake.

Haya wanasema yamechangiwa na hatua ya Raila Odinga kuingia kwenye mkataba wa handisheki na Rais mwezi Machi 2018.

Wawili hao wamekuwa wakishinikiza wandani wao kupitisha mswada wa BBI ambao unalenga kuleta mageuzi ya mfumo wa uongozi.

Hata hivyo, safari yao ilipata pigo baada ya majaji wa mahakama ya juu kusema mswada huo unaenda kinyume cha sheria.

Kutupiliwa kwa mswada huo kumechemsha ulingo wa kisiasa huku kila pande ikitoa hisia mseto kuhusu uamuzi wa majaji hao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke