Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco yatwaa ubingwa wa Afrika

94993 Pic+moroko Morocco yatwaa ubingwa wa Afrika

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

WENYEJI Morocco wametwaa ubingwa wa Afrika wa Futsal kwa kishindo baada ya kuifunga Misri mabao 5-0 katika mchezo wa fainali. Mbali ya kutetea ubingwa wake, ushindi huo ni wa pili kwa Morocco dhidi ya Misri ambao mwaka 2016, timu hiyo ilishinda mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika nchini Afrika Kusini. Morocco ilianza kwa kasi katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Ndani wa Al Hizam ingawa haikuwa kazi rahisi kwa Morocco kupata ushindi huo kutokana na upinzani mkali dhidi ya Misri ambayo ilicheza vizuri licha ya kuruhusu mabao hayo. Ikishangiliwa na mamia ya mashabiki, Morocco ilipata bao la kuongoza dakika ya tatu ya mchezo kupitia Soufiane El Mesrar akitumia vilivyo pasi ya Anas El Ayyane. Bao hilo lilionekana kuwapa nguvu Morocco na hasa aina ya ushangiliaji na uzomeaji wa mashabiki wao kwa timu pinzani na kupata bao la pili dakika ya 13 kupitia Abdeltif Fati baada ya kazi nzuri ya Achraf Saoud. Misri ambao walionekana kutobadilika licha ya kuwa nyuma kwa mabao mawili, waliendelea kulishambulia  lango la Morocco  huku wakikosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga huku Morocco iliandika bao la tatu dakika moja kabla ya mapumziko Kupitia El Mesrar. Kipindi cha pili kilikuwa na ushindani mkubwa ambapo Morocco ilikuwa inataka kulinda huku ikiongeza mabao ya kufunga na Misri ikitaka kusawazisha. Makosa ya walinzi wa Misri yaliipa faida Morocco na kufunga mabao mawili ambayo yalizamisha kabisa jahazi la wapinzani wao. Mabao ya Ayyane katika dakika ya 23 na Saad Knia dakika ya  27 yalifuta kabisa ndoto za Misri za kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne. Wakati huo huo; Angola iliifunga Libya 2-0 na kufuzu katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini Lithuania kuanzia Septemba 12 mpaka  Oktoba 4 mwaka huu. Mabao ya Angola yalifungwa na Athur Da Silva dakika ya 16 na  Magno Felipe Comes muda wa nyongeza yalitosha kuizamisha Libya kwenye mashindano hayo. Rais wa Caf, Ahmad Ahmad alimkabidhi kombe nahodha wa Morocco, Youssef  El Mazray huku kipa wa timu hiyo, akishinda tuzo ya mchezaji bora. Kipa huyo amefungwa bao moja tu tangu kuanza kwa mashindano huku mshambuliaji wa Angola Jose da Silva Magu akiibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao sita.

Chanzo: mwananchi.co.tz