Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco yanasa tani 1.4 za kokeni zilizofichwa kama ndizi

Morocco Yanasa Tani 1.4 Za Kokeni Zilizofichwa Kama Ndizi Morocco yanasa tani 1.4 za kokeni zilizofichwa kama ndizi

Wed, 3 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Morocco wamekamata tani 1.488 za kokeni katika operesheni ya pamoja na vikosi vya usalama vya Uhispania.

Kokeni hiyo ilipatikana ikiwa imefichwa kwenye masanduku ya ndizi ndani ya kontena katika meli inayotoka Amerika Kusini kuelekea Uturuki.

Ukamataji huo ulifanywa Jumanne katika bandari ya Tanger Med kaskazini mwa Morocco.

Mamlaka ya Morocco inasema wanashuku kokeini ilikuwa ikisafirishwa kama sehemu ya operesheni ya kimataifa ya ulanguzi wa dawa za kulevya lakini bado wanaendelea na uchunguzi.

Tukio hilo linakuja siku moja tu baada ya mamlaka kukamata karibu kilo 363 za kokeini katika lori lililokuwa likijaribu kuingia Morocco kupitia mpaka na Mauritania.

Nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika inaelezwa kuwa njia kuu ya kusafirisha dawa za kulevya kutoka Amerika Kusini hadi Ulaya.

Chanzo: Bbc