Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco yahalalisha ulimaji bangi kwa ajili ya biashara

Bangi Pic Data Morocco yahalalisha ulimaji bangi kwa ajili ya biashara

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: Bbc

Serikali ya Morocco imetoa vibali 10 kwa wakulima kulima bangi kihalali kwa ajili ya viwanda na kuuza nje kwa mara ya kwanza.

Wakulima katika maeneo ya kaskazini ya al-Hoceima, Chefchaouen na Taounate wataruhusiwa kuzalisha na kuuza bangi kwa matumizi ya kimatibabu, dawa na viwandani, kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na bunge mwaka jana.

Shirika la kitaifa linalodhibiti shughuli za bangi ambalo lilitoa vibali hivyo limesema wakulima watahimizwa kuongeza uzalishaji halali wa bangi ili kukidhi hitaji la soko.

Morocco kwa muda mrefu imekuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa bangi haramu ulimwenguni. Inakuzwa katika maeneo maskini zaidi ya milimani ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini na kusafirishwa kwenda Ulaya.

Hatua ya serikali ya kuhalalisha uzalishaji wa bangi inalenga kuboresha hali ya wakulima maskini na kuzalisha mapato kwa uchumi.

Chanzo: Bbc