Maellfu ya raia nchini Morocco wameandamana jijini Rabat wakitoa wito kwa mamlaka kusitisha uhusiano na Israeli kutokana na mapigano ya huko Gaza.
Inaelezwa kuwa wanasiasa mbalimbali kwenye taifa hilo waliungana na raia kwenye maandamano hayo.
Morocco ilianzisha uhusiano na nchi ya Israeli mwaka wa 2020 chini ya mazungumzo yalioongozwa na Marekani.
Upinzani dhidi ya makubaliano hayo umekuwa ukionekana tangu kuanza kwa vita huko Gaza.
Haya yanajiri wakati huu wizara ya afya huko Gaza inayoendeshwa na Hamas ikisema takriban watu 28,176 wameuawa na 67,784 wamejeruhiwa katika mashambulio ya Israel kwenye eneo hilo tangu Oktoba 7, idadi kubwa ya wanawake na watoto.
Maafisa wa Israel wanasema kuwa takriban watu 1,140 waliuawa katika mashambulio yaliyoongozwa na Hamas Oktoba 7 kusini mwa Israel.
Wapiganaji wa Hamas waliwateka watu 250 wakati wa shambulio hilo na 132 bado wanazuiliwa huko Gaza, kulingana na takwimu za Israeli.