Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moïse Katumbi apiga kura mjini Lubumbashi

 Katumbi Apiga Kura Mjini Lubumbashi Moïse Katumbi apiga kura mjini Lubumbashi

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: Bbc

"Nilikuja kupiga kura", haya yalikuwa maneno ya kwanza ya mgombea wa chama cha Ensemble pour la République, Moïse Katumbi, kwa BBC Afrika baada ya kura yake.

Gavana wa zamani wa Katanga ametimiza wajibu huu wa kiraia.

Alilakiwa na maelfu ya wafuasi katika mojawapo ya vituo vya kupigia kura mjini Lubumbashi.

"Hatuogopi chochote kabisa. Tutashinda chaguzi hizi,” anashangilia kabla ya kutoa wito kwa wafuasi wake kuwa macho.

"Lazima tufuatilie kura hadi mwisho. Lazima tuhesabu kituo cha kupigia kura kwa kituo cha kupigia kura. Matokeo pekee ambayo tutakubali ni yale yatakayooneshwa katika kila kituo cha kupigia kura,” anaonya.

Kama wagombea wengine wa upinzani ambao tayari wamepiga kura, Moïse Katumbi anashutumu dosari katika kuandaa kura hii.

Chanzo: Bbc