Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnigeria mashakani kwa kujaribu kuibia Telkom "credit" mara 58

0fgjhs7bbcsc2lkte Mnigeria mashakani kwa kujaribu kuibia Telkom "credit" mara 58

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mnigeria huyo alisajili laini 14 za simu ambazo alizitumia katika njama ya kuiba muda wa maongezi ili kuwauzia wateja pesa taslimuBancho aliachiliwa kwa dhamana ya KSh100,000 pesa taslimu, bado anaendelea kuchunguzwaKorti ilimuagiza Mnigeria huyo awasilishe wadhamini wawili raia wa Kenya ambao watakuwa wanahakikisha anafikishwa kortini

Polisi jijini Nairobi wanamchunguza raia mmoja wa Nigeria kwa kujaribu kuibia Kampuni ya Mawasiliano ya Jamii Telkom muda wa maongezi mara 58.

Licha ya mtuhumiwa Tokundo Abiondun Bancho kuachiliwa kwa dhamana ya KSh100,000 pesa taslimu, bado anaendelea kuchunguzwa.

Hakimu Mwandamizi Caroline Njagi alimuagiza Bancho awasilishe wadhamini wawili raia wa Kenya ambao watakuwa wanahakikisha mshukiwa huyo anafikishwa kortini, kama ilivyoripoti gazeti la Taifa Leo, Ijumaa, Julai 30.

Korti ilifahamishwa kuwa Mnigeria huyo alisajili laini 14 za simu ambazo alizitumia katika njama ya kuiba muda wa maongezi ili kuwauzia wateja pesa taslimu.



Read also

Mumewe Caroline Kangogo Aomba Kutowahutubia Waombolezaji

Katika uamuzi wake, Hakimu Njagi alimuagiza Bancho awe akiripoti katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga kila siku.

Bancho anatarajiwa kurudishwa kortini mnamo Agosti 12, 2021. ambapo atafunguliwa mashtaka ya kupanga njama ya uhalifu ya kuiba KSh100,000.

Wawili wakamatwa kuhusiana na wizi wa Benki ya Equity, MatuuKatika taarifa nyingine ya uhalifu, maafisa wa upelelezi kaunti ya Machakos wamewatia nguvuni wahudumu wawili wa boda boda wanaoshukiwa kuhusika na wizi katika benki ya Equity tawi la Matuu siku ya Jumanne, Julai 27.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda mkuu wa polisi kaunti hiyo Issa Mohammud alisema wawili hao waliwasaidia majambazi katika kuvamia benki hiyo na kuiba kiwango kisichojulikana cha pesa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mohammud alisema polisi wana taarifa muhimu ambazo zitawasaidia kuwamata majambazi hao watano ambao pia wanadaiwa kuiba bunduki aina ya AK 47 kutoka kwa afisa wa polisi waliokuwa wanalinda lango la benki hiyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua mbayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690



Read also

Magazeti Jumatano, Julai 28: Mt Kenya Waahidi Kulipa Deni la Raila 2022

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke