Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmoja afariki, 11 wajeruhiwa baada ya jengo la mochwari kuporomoka Vihiga

C4824b770ecb4ef6 W Mmoja afariki, 11 wajeruhiwa baada ya jengo la mochwari kuporomoka Vihiga

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Lango la jengo hilo la kisasa lenye thamani ya mamilioni ya pesa liliporomoka Jumapili, Aprili 25, mwendo wa saa tisa alasiri

- Waashi 38 hawakuwa wanafahamu hatari hiyo wakati walikuwa kwenye eneo la ujenzi

- Jengo hilo lilizinduliwa na gavana wa kaunti hiyo Wilber Ottichilo, mnamo Februari 24

Hifadhi ya maiti ya kaunti ya Vihiga ambayo ilikuwa inajengwa iliporomoka na kumuua mwashi mmoja papo hapo na kuwaacha wengine 11 na majeraha mabaya.

Lango la jengo hilo la kisasa lenye thamani ya mamilioni ya pesa liliporomoka Jumapili, Aprili 25, mwendo wa saa tisa alasiri mjini Mbale.

Kulingana na mkuu wa mawasiliano wa kaunti hiyo, waashi 38 hawakuwa wanafahamu hatari hiyo wakati walikuwa kwenye eneo la ujenzi.

Waathiriwa 11 ambao walijeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Vihiga huku mmoja akiwa katika hali mahututi.

Mwili wa marehemu ulihifadhiwa kwenye makafani ya hospitali hiyo.

Japo sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo haijatajwa, wakazi wenye hamaki walidai kuwa ilitokana na msingi dhaifu na kuwaelekezea kidole cha lawama maafisa wa kaunti.

"Msingi wa ujenzi huo ni mbovu na kushangaza endapo kandarasi hiyo ilipewa mhandisi," mmoja wa mashahidi alidokezea TUKO.co.ke.

Jengo hilo lilizinduliwa na gavana wa kaunti hiyo Wilber Ottichilo, mnamo Februari 24.

Katika taarifa tofauti, watu kadhaa walikwama baada ya jengo kuporomoka katika wadi ya Kapkugerwet, Kaunti Ndogo ya Ainamoi, Kericho usiku wa Jumanne, Juni 9, 2020.

“Tebsview Building, inayomilikiwa na mkandarsi wa Kericho Charles Chaglano liliporomoka baada ya saa moja unusu usiku," alisema afisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kericho, Sofia Tuwei kama alivyonukuliwa na Daily Nation.

Mtoto wa miaka sita aliripotiwa kupoteza maisha yake huku wengine wakiokolea kutoka kwa vifusi.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke