Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmiliki chumba cha maiti akiri kuuza viungo vya binadamu

Mmiliki Maiti Mmiliki chumba cha maiti akiri kuuza viungo vya binadamu

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: BBC

Mmiliki wa zamani wa chumba cha kuhifadhiamaiti huko Colorado alikiri shtaka Jumanne kwa kwa kuwalaghai jamaa za wafu kwa kupasua maiti za wanafamilia wao na kuuza sehemu za miili yao bila ruhusa, tabia iliyofichuliwa katika ripoti ya uchunguzi ya Reuters ya 2018.

Kulingana na Reuters, Megan Hess ambaye ambaye alisimamia chuma hicho cha mazishi kwa jina Sunset Mesa na biashara ya viungo vya mwili wa binadamu iitwayo Donor Services kutoka jengo moja, aliingia katika shauri la shtaka la ulaghai katika kesi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Marekani Gordon Gallagher huko Grand Junction, Colorado.

Gallagher alipanga Hess, ambaye hapo awali alikana mashtaka, kuhukumiwa mwezi Januari, na upande wa mashtaka ukitaka kifungo cha miaka 12 hadi 15 jela.

Hess, mwenye umri wa miaka 45, alikiri Jumanne kwamba kupitia nyumba yake ya mazishi, iliyoko katika mji wa Montrose katika sehemu ya magharibi ya jimbo hilo, alilaghai angalau familia kumi na mbili zinazotafuta huduma za kuchoma maiti kwa jamaa waliokufa.

Badala ya kuchoma maiti, rekodi za mahakama zinaonyesha, kampuni yake ya wakala ilivuna vichwa, mikono na miguu na kisha kuviuza, hasa kwa mafunzo ya upasuaji na madhumuni mengine ya kielimu.

Hess alikuwa ameratibiwa kuhukumiwa baada ya wiki tatu pamoja na mamake, Shirley Koch, ambaye hapo awali alikana mashtaka. Kesi ya mabadiliko ya rufaa ya Koch imepangwa Julai 12.

Baada ya Wakili Msaidizi wa Marekani Jeremy Chaffin kutoa pendekezo lake la hukumu, wakili wa Hess, Dan Shaffer, alihimiza kifungo chepesi cha takriban miaka miwili jela. Hess amekuwa huru kwa dhamana tangu kukamatwa kwake.

Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo, hakimu alimtaka Hess aeleze kwa maneno yake uhalifu aliofanya. Hapo awali Hess aliita suala zima "uharibifu wa kisheria." Alipotakiwa na hakimu kujieleza kujieleza, Hess alikubaliana na upande wa mashtaka aliwalaghai wahasiriwa wake, ingawa alikataa kuelezea kwa undani.

Chanzo: BBC