Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu waikumba Sudan

Kipindupindu Chasababisha Vifo Vya Watu 10 Afrika Kusini Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu waikumba Sudan

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban visa 817 vinavyoshukiwa kuwa maradhi ya kipindupindu vimeripotiwa katika majimbo matatu ya Sudan, vikiwemo vifo 35.

Visa hivyo viliripotiwa katika majimbo ya Gedaref, Kordofan Kusini na Khartoum, tovuti ya habari inayomilikiwa kibinafsi ya al-Rakoba iliripoti, ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulisema kuwa miezi kadhaa ya migogoro nchini Sudan imewaacha mamilioni ya watu katika hatari ya ugonjwa wa kipindupindu, surua, malaria na magonjwa mengine bila uwezo wa kutosha wa kujizuia.

WHO pia imeonya kwamba maisha ya zaidi ya wagonjwa 9,000 wa figo yako hatarini kutokana na idadi ndogo ya vituo vya kusafisha damu nchini humo.

Hospitali za Sudan zimeathiriwa pakubwa na mzozo kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi, huku nyingi zikisimamisha shughuli huku kukiwa na mapigano.

Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000 na wengine karibu milioni sita kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live