Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko wa Ebola wamalizika rasmi Congo

Ebola Case23 Mlipuko wa Ebola wamalizika rasmi Congo

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlipuko wa hivi punde wa Ebola umedhibitiwa ndani ya miezi mitatu kutokana na "mwitikio wa haraka" na "madhubuti" katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linasema Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Watu wanne wamefariki tangu mlipuko huo wa 14 nchini humo tangu 1976 kutangazwa mwezi Aprili katika mji wa magharibi wa Mbandaka.

Watatu kati ya waliokufa walichukuliwa kuwa "kesi zilizothibitishwa" na mmoja alichukuliwa kuwa kesi shirika la afya ulimwenguni lilisema.

Shirika la Umoja wa Mataifa lilifanya kazi pamoja na serikali kusambaza chanjo, upimaji, ufuatiliaji,kuzuia na kudhibiti maambukizi, pamoja na ushirikishwaji wa jamii.

"Matokeo haya yanaonyesha kuimarisha utayari, ufuatiliaji wa magonjwa na ugunduzi wa haraka, kupiga hatua mbele," Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika Dk Matshidiso Moeti alisema katika taarifa yake Jumatatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live