Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko mkubwa waua 2 na kujeruhi 77 jimbo la Oyo, Nigeria

Oyo, Nigeria Mlipuko mkubwa waua 2 na kujeruhi 77 jimbo la Oyo, Nigeria

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wameuawa na wengine 77 kujeruhiwa baada ya mlipuko mkubwa kutikisa makumi ya majengo usiku wa kuamkia leo katika mojawapo ya miji mikubwa zaidi ya Nigeria.

Hayo yamesemwa leo na gavana wa mji wa Ibadan wakati waokoaji wakichimba vifusi kutafuta watu wanaohofiwa kukwama ndani ya vifusi hivyo.

Wakazi wa mji wa Ibadan wenye idadi kubwa ya watu katika jimbo la kusini-magharibi la Oyo wamesema mlipuko mkubwa ulisikika mwendo wa saa 7:45 usiku, na kusababisha hofu huku wengi wakikimbia makazi yao.

Mapema leo Jumatano, askari usalama walizingira eneo hilo huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Gavana wa Oyo, Seyi Makinde, amewaambia waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo la Bodija huko Ibadan kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huo umesababishwa na baruti zilizohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya uchimbaji haramu wa madini.

Uchimbaji haramu wa madini katika nchi ya Nigeria yenye utajiri wa madini ni jambo la kawaida na limekuwa tatizo kubwa kwa serikali ya nchi hiyo. Shughuli hizo hufanyika katika maeneo ya mbali ambako ni vigumu kwa wahalifu kukamatwa, na taratibu za usalama hazizingatiwi.

Gavana Makinde amesema: "Uchunguzi unaendelea na wote watakaopatikana na hatia watafikishwa mahakamani."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live