Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko mbaya waathiri vitongoji kadhaa vya jiji la Nigeria

Mlipuko Mbaya Waathiri Vitongoji Kadhaa Vya Jiji La Nigeria Mlipuko mbaya waathiri vitongoji kadhaa vya jiji la Nigeria

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mlipuko mkubwa uliotokea katika mji wa Ibadan nchini Nigeria umeua watu wawili na kuwajeruhi wengine 77 usiku kucha.

Juhudi za uokoaji zinaendelea katika vitongoji saba vya jiji la tatu kwa idadi kubwa ya watu nchini Nigeria.

Chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika, lakini mamlaka inashuku kuwa huenda ulichochewa na vilipuzi vya uchimbaji madini vilivyohifadhiwa ndani ya nyumba.

Picha zinaonyesha majengo yamegeuzwa kuwa vifusi na magari yaliyoharibiwa na mlipuko.

Video zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, huku shahidi mmoja akielezea duka moja kuharibiwa katika eneo la Bodija, wilaya ya makazi ya jiji hilo.

"Tunasikia kishindo kikubwa mwendo wa 07:30pm. Dominoes Pizza na Ace Mall huko Bodija ziliharibiwa," alisema.

Polisi wameahidi uchunguzi wa haraka kuhusu mlipuko huo.

"Uchunguzi wa awali wa vyombo vya usalama umebaini kuwa wachimbaji haramu waliokuwa wakimiliki moja ya nyumba za Bodija walikuwa wamehifadhi vilipuzi vilivyosababisha mlipuko huo," mkuu wa mkoa huo Seyi Makinde alisema.

Chanzo: Bbc