Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko kwenye ghala la mafuta Guinea

Motoossm Mlipuko kwenye ghala la mafuta Guinea

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika mji mkuu wa Guinea (Conakry) kufuatia mlipuko uliotokea katika ghala la mafuta katika kitongoji cha Kaloum, Guinea

Mlipuko huo umetokea alfajiri ya leo Jumatatu ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa takribani watu wanne wamefariki na wengine 100 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

“Ndiyo, kuna vifo na majeruhi,” afisa mkuu wa polisi aliambia shirika la habari la Reuters, akiongeza kuwa bado wanahesabu idadi ya vifo na majeruhi.

Hospitali kuu mbili za Conakry, Ignace Deen na Donka zimejaa watu wengi waliojeruhiwa katika tukuo hilo, ambapo pia Mlipuko huo umesababisha uharibifu mkubwa na kuwalazimu makundi kadhaa ya watu kukimbia.

Hata hivyo, tayari polisi wamezuia eneo la bandari huku jeshi la zima moto likiwa limeshafika katika eneo la mlipuko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live