Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko Nairobi: 'Msimamizi aligonga milango ya kila mtu kwa hasira'

Mlipuko Nairobi: 'Msimamizi Aligonga Milango Ya Kila Mtu Kwa Hasira' Mlipuko Nairobi: 'Msimamizi aligonga milango ya kila mtu kwa hasira'

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Wakaazi wa eneo la makazi la Mradi huko Embakasi, Kusini Mashariki mwa Nairobi wameelezea kushuhudia matukio ya kutisha ya vitu vya chuma vilivyoruka ikiwa ni pamoja na sehemu za gari, mitungi ya gesi na kontena la usafirishaji kufuatia mlipuko mkubwa.

Jackline Karimi mwenye umri wa miaka thelathini na tano aliambia BBC alikimbia nje ya nyumba na kulala kwenye lami, hatua ambayo huenda ilimuokoa.

Alipata majeraha ya moto kwenye mkono wa kulia hadi begani na mguu wa kulia.

"Nilimwona mwanamke akiwaka moto lakini hatukuweza kumsaidia. Kila mtu alikuwa akikimbia."

Jackline alisema amesikia kuwa mwanamke huyo alifariki kutokana na majeraha yake.

Mlipuko wa kwanza ulipotokea Jackline alisema kwamba mlinzi wa jengo hilo aligonga milango kwa hasira na kuwaamuru wakaazi watoke nje.

"Watu walikuwa wakipiga kelele na wengine wakipiga kelele 'moto!'," Jackline alisema."Gesi ilikuwa inawaka katika sehemu tofauti ikichoma chochote ilichopata njiani."

Chanzo: Bbc