Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko Nairobi: Mamlaka ya kuthibiti Kawi Kenya (EPRA) ilikataa kutoa kibali cha ujenzi

Mlipuko Nairobi: Mamlaka Ya Kuthibiti Kawi Kenya (EPRA) Ilikataa Kutoa Kibali Cha Ujenzi Mlipuko Nairobi: Mamlaka ya kuthibiti Kawi Kenya (EPRA) ilikataa kutoa kibali cha ujenzi

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka ya kuthibiti kawi nchini Kenya (EPRA) imesema ilikataa kutoa kibali cha ujenzi wa kiwanda cha kujaza na kuhifadhi mitungi ya gesi ya kupikia katika eneo ambako mlipuko mkubwa umetokea jana usiku na kuua watu watatu huku wengine takriban 300 wakijeruhiwa.

Kupitia taarifa, EPRA imesema ilipokea ombi la ujenzi wa kiwanda hicho tarehe 19 Machi 2023, Juni 20, 2023 na tarehe 31 Julai 2023 lakini maombi hayo yote yalikataliwa baada ya muombaji wa leseni kushindwa kuthibitisha mikakata ya kuwahakikishia usalama wakaazi wengi wanaoishi katika eneo hilo na pia kushindwa kutoa tathmini ya hatari ya kiwanda hicho kuwepo katika eneo la makazi.

EPRA imesema uchunguzi wao kuhusu kilichotokea utasaidia kuvumbuachanzo cha mlipuko huo. .

Chanzo: Bbc