Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlinzi wa Odinga adaiwa kutekwa

Raila Odinga Kuongoza Maandamano Dhidi Ya Serikali Ya Rais Ruto Mlinzi wa Odinga adaiwa kutekwa

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Upinzani nchini Kenya ODM kimedai kuwa mlinzi wa kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga anayejulikana kwa jina la Maurice Ogeta amedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa maafisa wa polisi.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatano Julai 19, 2023 na chama hicho, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ODM, Philip Etale amedai, Ogeta alivamiwa na watu wasiojulikana alipokuwa akielekea kazini kutoka nyumbani kwake leo asubuhi ambao walimshusha kwenye gari yake na kisha kumfunga na kumuweka kwenye buti ya gari yake.

Etale amedai kuwa baada ya dakika chache, gari ilisimama na wavamizi walimtoa Ogeta kwenye buti na kumlazimisha kuwasaidia kuwasha gari hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live