Thu, 8 Feb 2024
Chanzo: Bbc
Watu wanaopanda Mlima Everest sasa watalazimika kusafisha kinyesi chao wenyewe na kukirejesha kwenye kambi ya msingi ili kutupwa, mamlaka imesema.
"Milima yetu imeanza kunuka," Mingma Sherpa, mwenyekiti wa manispaa ya kijijini ya Pasang Lhamu, aliiambia BBC.
Manispaa, ambayo inashughulikia eneo kubwa la Mlima Everest, imeanzisha sheria mpya kama sehemu ya hatua nyingi zinazotekelezwa.
Kwa sababu ya halijoto kali, kinyesi kinachoachwa kwenye Mlima Everest hakiharibiki kikamilifu.
Chanzo: Bbc