Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlevi afurumusha mawe kituo cha polisi, amjeruhi askari

Mawe Polisii Askari Polisi

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waswahili wana msemo wa kwamba 'Pombe sio chai wala juisi' hivyo ukiwa unamwagilia moyo kumbuka kunywa kistaarabu kwani matokeo yake unaweza kuyashangaa hata wewe uliyekunywa na kufanya kitendo hicho.

Polisi katika eneo la Solai lililopo kaunti ya Nakuru nchini Kenya wanamshikilia Dennis Kibet kwa kosa la kuwashambulia askari wa Jeshi hilo kwa mawe wakati akiwa amelewa mbwii.

Ripoti iliyotolewa na Jeshi la Polisi wa eneo hilo imeeleza kuwa Dennis alikuwa katika hali ya ulevi na kuanza kurusha mawe katika kituo cha polisi tukio lililopelekea kumjeruhi na kumtegua bega Askari Eliud Misiko.

Baada ya kuulizwa Mtuhumiwa huyo alijibu kuwa alitaka kuona kuwa akirusha mawe katika kituo cha polisi kutatokea kitu gani.

Kitendo hicho kimefanya ashikiliwe akisubiri kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kushambulia Polisi pamoja na kukutwa na bangi. #TanzaniaWeb.com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live