Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa zamani shirikisho la soka barani Afrika afariki akiwa na umri wa miaka 77

Mkuu Wa Zamani Shirikisho La Soka Barani Afrika Afariki Akiwa Na Umri Wa Miaka 77.png Mkuu wa zamani shirikisho la soka barani Afrika afariki akiwa na umri wa miaka 77

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Aliyekuwa rais wa muda mrefu wa Shirikisho la Soka Afrika, Issa Hayatou amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Raia huyo wa Cameroon alihudumu kwa miaka 29 kama katika shirikisho hilo linaloongoza soka barani Afrika, na alikuwa urais mnamo wake kuanzia mwaka 1988 hadi alipoondoka madarakani mnamo mwaka 2017.

Pia alishika nyadhifa za juu ndani ya shirikisho la soka duniani Fifa.

Hayatou alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya shirikisho hilo lenye makao yake Uswizi, ambalo sasa linajulikana kama baraza la Fifa, kuanzia 1990 hadi 2017.

Alihudumu muda mfupi kama kaimu rai swa Fifa kati ya mwaka 2015 na 2016 baada ya Sepp Blatter kusimamishwa kazi.

Rais wa Fifa Gianni Infantino alitoa pongezi kwa Hayatou, ambaye katika ujana wake alikuwa mwanariadha wa mbio na mchezaji wa mpira wa vikapu, katika chapisho kwenye Instagram.

"Imenisikitisha kusikia kifo cha aliyekuwa rais wa Caf, aliyekuwa rais wa muda wa Fifa, makamu wa rais wa Fifa na mjumbe wa baraza la Fifa, Issa Hayatou," Infantino aliandika.

"Alikuwa shabiki wa michezo, alijitolea maisha yake katika usimamizi wa michezo.

"Kwa niaba ya Fifa, rambirambi ziende kwa familia yake, marafiki, wafanyakazi wenzake wa zamani na wote wanaomfahamu. Pumzika kwa amani."

Agosti 2021 Hayatou alipigwa marufuku ya mwaka mmoja kwa kukiuka kanuni zake za maadili wakati wa kusaini mkataba mkubwa zaidi kuwahi kutokea barani Afrika na kampuni ya habari ya Ufaransa ya Lagardere mnamo 2016.

Adhabu hiyo hata hivyo ilibatilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa michezo mnamo mwezi Februari mwaka uliofuata.

Chanzo: Bbc