Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa ujasusi M23 auawa katika shambulio la ndege DRC

Ujajusi M23 Mkuu wa ujasusi M23 auawa katika shambulio la ndege DRC

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa kitengo cha ujasusi wa kundi la waasi la M23 ameripotiwa kuuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maafisa wamefichua kwamba, Kanali Castro Elise Mberabagabo aliuawa jana Jumanne katika shambulio la vikosi vya jeshi la Congo kwenye kambi ya M23 huko Kitchanga, eneo la Masisi.

Wenyeji wa eneo hilo wamesema walisikia milipuko mikubwa huku wanajeshi wa Congo DR wakifanya shambulio la kushtukiza dhidi ya ngome ya waasi katika katika eneo hilo.

Chanzo kimoja kimesema, Mberabagabo aliwahi kuwa Afisa Uhusiano wa Nje wa M23, na kwamba mauaji yake ni hasara kubwa kwa kundi la waasi la M23 kwa sababu amekuwa mhimili wa kundi hilo. Wapiganaji wa M23

Kanali Castro Elise Mberabagabo ambaye alikuwa na uraia wa Uingereza na ameoa Muingereza, pia alikuwa miongoni mwa wafadhili wakuu wa kundi la waasi la M23 kupitia mikataba ya dhahabu inayofanyika huko Mashariki mwa Congo.

Mberabagabo anayejulikana sana kama Castro, alimiliki mali na nchini Uganda, London na DRC.

Hivi majuzi ChimpReports iliripoti kuwa vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimenunua makumi ya ndege zisizo na rubani kutoka China ili kukabiliana na tishio la waasi wa M23.

Ndege zisizo na rubani zimekuwa changamoto kubwa kwa makundi ya waasi ambayo katika muongo mmoja uliopita yamekuwa yakitumia mbinu ya vita vya msituni ili dhidi ya jeshi la serikali ya Congo DR.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live