Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa polisi wa Haiti yuko Kenya kabla ya kupambana na magenge

Mkuu Wa Polisi Wa Haiti Yuko Kenya Kabla Ya Kupambana Na Magenge Mkuu wa polisi wa Haiti yuko Kenya kabla ya kupambana na magenge

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Mkuu wa polisi wa Haiti Frantz Elbe yuko nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu kabla ya mipango ya kupeleka polisi kusaidia kupambana na ghasia za magenge katika nchi hiyo ya Caribbean.

Bw Elbe na ujumbe wake Jumatano walikutana na mkuu wa polisi wa Kenya Japhet Koome na maafisa wengine wakuu wa usalama kwa ajili ya "majadiliano ya usalama wa nchi mbili", Huduma ya Polisi ya Kitaifa ya Kenya ilisema.

Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kutumwa kwa zaidi ya maafisa wa polisi 1,000 kutoka Kenya kwa ajili ya Ujumbe wa Kimataifa wa Kusaidia Usalama (MSS), Umoja wa Mataifa uliidhinisha miezi miwili iliyopita, kulingana na vyombo vya habari vya Kenya.

Kikosi cha kwanza cha maafisa wapatao 300 kimepangwa kutumwa ifikapo Februari mwaka ujao, kulingana na gazeti la kibinafsi la The Star.

Mwezi uliopita, bunge la Kenya liliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao, lakini mahakama kuu ilirefusha amri ya kuzuia hatua hiyo, ikisubiri matokeo ya pingamizi la kisheria katika mpango huo.

Mpango huo umekabiliwa na ukosoaji mkubwa, hasa kutokana na rekodi mbaya ya hatua za awali nchini Haiti na rekodi ya ukiukwaji wa haki na polisi wa Kenya.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amelaani mpango huo lakini Rais William Ruto ameutetea akisema kuwa; “Afrika ina nia ya kuchangia uhuru na usalama wa Haiti”.

Karibu magenge 300 yanafanya kazi kote Haiti na 80% ya mji mkuu, Port-au-Prince, iko chini ya udhibiti wa magenge.

Chanzo: Bbc