Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa jeshi la Sudan akataa maridhiano na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)

Jeshi La Sudan Ladai Kupiga Hatua Kubwa Katika Vita Dhidi Ya RSF Mkuu wa jeshi la Sudan akataa maridhiano na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan ambaye pia ni Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF), Abdel Fattah Al-Burhan amesema kuwa, jeshi lake litaendelea kupambana na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na hakuna mapatano yoyote yaliyofikiwa.

Al-Burhan amesema katika hotuba yake ya kwa njia ya video iliyosambazwa jana Ijumaa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram na kusisitiza kwa kusema: "Hakuna maridhiano wala makubaliano tuliyofikia na waasi. Tutapigana hadi wanamgambo wakome, au sisi tukome."

Aidha amesema: "Vita vyetu vitaendelea hadi kila eneo la Sudan litakapokombolewa."

Mkuu huyo wa jeshi la Sudan amepongeza kampeni maalumu iliyoanzishwa nchini hhumo chini ya anwani ya "Sudanese Popular Resistance" na kusema: "Tunakaribisha upinzani wa wananchi, na tutawapa silaha, lakini silaha lazima zihalalishwe na kusajiliwa na jeshi."

Vilevile amelalamikia tamko lililotiwa saini hivi karibuni kati ya RSF na muungano wa kisiasa wa Uratibu wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Wananchi (Taqaddum) ambao unaongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan Abdalla Hamdok.

Amesema: "Wanasiasa waliotia saini makubaliano na RSF wamefanya makosa kwa kuzungumza na waasi. "Makubaliano ya wanasiasa na RSF hayakubaliki na hayana thamani yoyote," amesema.

Tarehe pia mwezi huu wa Januari 2024, Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF na muungano wa kisisa wa Taqaddum walitia saini "Azimio la Addis Ababa" ili kukomesha vita na mapigano nchini Sudan.

Kwa mujibu wa tamko hilo, RSF iko tayari kusitisha vita mara moja na bila ya masharti yoyote kupitia mazungumzo ya moja kwa moja na jeshi la Sudan.

Katika upande mwingine, serikali ya Sudan juzi Alkhamisi ilimwita nyumbani balozi wake wa mjini Nairobi kwa mashauriano, ikiwa ni kupinga hatua ya Rais wa Kenya, William Ruto, ya kumkaribisha na kumpokea nchini humo Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live