Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa jeshi la Sudan aelekea Misri safari ya kwanza tangu Aprili

 Mkuu Wa Jeshi La Sudan Aelekea Misri Safari Ya Kwanza Tangu Aprili Mkuu wa jeshi la Sudan aelekea Misri safari ya kwanza tangu Aprili

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Maafisa nchini Sudan wanasema mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameondoka nchini humo kuelekea Misri kukutana na Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Hii ni mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa kijeshi wa Sudan kuondoka nchini humo tangu mzozo ulipozuka mwezi wa Aprili, kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces (RSF).

Rais wa Misri amemuunga mkono Jenerali Burhan wakati wa vita hivyo ambavyo Umoja wa Mataifa unasema sasa vimewalazimu zaidi ya Wasudan milioni nne kuyakimbia makazi yao.

Hadi siku chache zilizopita kiongozi wa kijeshi wa Sudan alikuwa amejificha ndani ya makao makuu ya jeshi huko Khartoum.

Ukweli kwamba Jenerali Burhan sasa ameweza kuondoka nchini humo kwa mazungumzo na mshirika wake nchini Misri ni kwa baadhi ya ishara kwamba jeshi liko chini ya shinikizo kidogo.

Wanamgambo wa RSF huenda wamedhoofishwa katika mji mkuu. Lakini huko Darfur RSF bado ina nguvu na imekuwa ikifanya mashambulizi ya kikabila.

Chanzo: Bbc