Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa jeshi la Kenya aliyefariki katika ajali ya helikopta kuzikwa leo

Mkuu Wa Jeshi La Kenya Aliyefariki Katika Ajali Ya Helikopta Kuzikwa Leo.png Makamu wa Rais awataka viongozi wa vyuo kuandika vitabu vya kuielezea Tanzania

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa majeshi nchini Kenya, Jenerali Francis Ogola aliyefariki alahamisi 18 Aprili atazikwa leo nyumbani kwake katika kaunti ya Siaya magharibi mwa Kenya.

Jenerali Ogola alifariki katika ajali ya ndege, iliyotokea katika eneo la Kabem, Elgeyo Marakwet kwenye bonde la ufa.

Mwili wake Jenerali umewasili katika eneo la Ng'iya kwenye eneo bunge la Alego Usonga na utafikishwa katika shule ya upili ya Seneta Obama ambapo ibada ya wafu itaandaliwa kabla ya maziko yake baadaye leo.

Gwaride la kuuaga mwili wake linaandaliwa na jeshi la wanahewa. Jenerali Ogola alikuwa rubani wa kivita katika jeshi la angani.

Kulingana na taratibu za kijeshi na jinsi alivyotaka mwenyewe na kunakili katika wasifu wake, Jenerali atazikwa baada ya ibada fupi itakayoongozwa na viongozi wa kidini wa kiraia wakisaidiana na wale wa kijeshi.

Baada ya ibada hiyo, wanajeshi watamsindikiza jenerali wao, kwa gwaride itakayoongozwa na bendi ya mseto ya vikosi vyote vitatu vya kijeshi.

Msafara utakapofika nyumbani kijijini Mor, tarumbeta zitapigwa kuashiria kwamba mwanajeshi amefariki vitani, kwa kiingereza inafahamika kama Reville, tarumbeta hii itakuwa yenye kupigwa haraka kiasi…baada ya hapo kutakuwa na dakika moja ya kunyamaza kumuomboleza marehemu na kisha kufuatiwa na tarumbetea nyingine itapigwa inayofahamika kama THE LAST POST…hii itapigwa kwa utaratibu na kwa muda, kuashiria kwamba safari yake mwanajeshi kazini imekamilika na kwamba ni hali ya kumpa mkono wa buriani.

Bendera ya kitaifa ambayo aliitumikia kazini jenereali itakunjwa na kukabidhiwa mjane wake, huku mizinga 19 ikipigwa na jeshi la wanamaji kama saluti ya mwisho kwa kiongozi wao.

Baada ya itifaki hizi, mwili wake utawekwa kaburini na kikosi cha majenereali wenzake ambao waliubebea mwili wake kwa siku zote tatu tangu kufariki kwake.

Jumapili hii ikikamilisha siku tatu za maombolezi ya kifo cha jenerali Ogola ambapo bendera ya kitaifa, za kijeshi na ile ya EAC zikipeperushwa nusu mlingoti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live