Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa jeshi Algeria afa kwa mshtuko wa moyo

89794 Algeria+pic Mkuu wa jeshi Algeria afa kwa mshtuko wa moyo

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mkuu wa jeshi nchini Algeria, Gaid Salah amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo.

Rais mpya wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa na siku saba kwa jeshi kutokana na kifo cha ghafla cha Salah, aliyekuwa na umri wa miaka 80.

Shirika la habari la serikali ya Algeria, APS, limeripoti kuwa Salah alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa nyumbani na kisha akapelekwa katika hospitali ya kijeshi.

Salah alionekana kuwa na ushawishi mkubwa katika kujiuzulu kwa Rais Abdelaziz Bouteflika Aprili mwaka huu, akiongeza mbinyo kwa kiongozi huyo wa muda mrefu baada ya maandamano ya umma nchini humo.

Katika miezi iliyofuata, Salah alikaidi masharti ya waandamanaji kuwa pia naye ajiuzulu. Aliunga mkono uchaguzi ulioandaliwa mwezi huu, ambao ulimweka madarakani Abdelmadjid Tebboune.

Chanzo: mwananchi.co.tz