Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa benki kuu ya Burundi aliyefutwa kazi akamatwa

D1c25c11 E8e7 4f2a 9dd0 E37e5615c763 Mkuu wa benki kuu ya Burundi aliyefutwa kazi akamatwa

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Gavana wa benki kuu ya Burundi aliyefutwa kazi hivi majuzi amekamatwa kwa tuhuma za ufisadi.

Dieudonné Murengerantwari ameshutumiwa na wizara ya sheria kwa "kuhujumu utendakazi mzuri wa uchumi wa taifa, ufisadi wa kimya kimya, ufujaji wa pesa na ufujaji wa mali ya umma".

Hajajibu tuhuma zinazomkabili.

Siku ya Jumapili, Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye alimfukuza kazi Bw Murengerantwari na nafasi yake kuchukuliwa na Édouard Normand Bigendako.

Bw Murengerantwari alikuwa ameteuliwa kuongoza benki kuu ya Burundi kwa miaka mitano kuanzia Agosti mwaka jana.

Mwanasheria Mkuu Leonard Manirakiza Jumanne alisema kuwa madai dhidi ya Bw Murengerantwari ni ya muda huku uchunguzi ukiendelea.

Pia alisemautaratibu wa sheria unafuatwa huku Bw Murengerantwari akiendelea kuzuiliwa.

Chanzo: Bbc