Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa WHO aonya juu ya kuchelewa ‘kuzuia mauaji ya halaiki’ huko Tigray

FfgLXH7XEAEjyTx.jpeg Mkuu wa WHO aonya juu ya kuchelewa ‘kuzuia mauaji ya halaiki’ huko Tigray

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema kuwa ‘’kuna muda kidogo sana wa kuzuia mauaji ya halaiki’’ katika eneo la nyumbani kwake la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Tedros, ambaye hapo awali aliwahi kuwa waziri wa afya wa Ethiopia na waziri wa mambo ya nje, amekuwa akikosoa vikali viongozi wa Ethiopia katika kipindi chote cha miaka miwili ya vita.

Katika maoni yake makali zaidi juu ya vita bado, Tedros aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva Jumatano kwamba chakula na huduma za afya zilikuwa zinatumika kama silaha za vita huko Tigray, ambayo kwa kiasi kikubwa imetengwa na ulimwengu wa nje.

‘’Hakuna hali nyingine ulimwenguni ambapo watu milioni sita wamezingirwa kwa karibu miaka miwili,’’ Tedros alisema.

Kuna muda mchache sasa kuzuia mauaji ya halaiki.’’

Mzozo nchini humo ulianza Novemba 2020 wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipotuma wanajeshi huko Tigray baada ya kukishutumu chama tawala cha eneo hilo cha Tigray People’s Liberation Front kwa kushambulia kambi za jeshi la shirikisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live