Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa RSF atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati

Mkuu Wa RSF Atoa Wito Kwa Jumuiya Ya Kimataifa Kuingilia Kati Mkuu wa RSF atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Tumepata na maoni mapya kutoka kwa mmoja wa wanaume wawili wanaohusika katika mzozo mkali ambao umeikumba Sudan .

Kamanda wa Kikosi Maalum cha Wanajeshi (RSF) Jenerali Mohammed Hamdan Daglo (pia anayejulikana kama Hemeti) ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati.

Katika jumbe za Twitter zilizotumwa asubuhi ya leo, anatoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya "uhalifu" wa mpinzani wake, kiongozi wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.Anadai kuwa wanajeshi wake wanapigana dhidi ya "Waislamu wenye itikadi kali".

Mkuu wa RSF anasema vita anavyoendesha ni "gharama ya demokrasia".

Anasema askari wake "hawakushambulia mtu yeyote" na wanajibu tu "kuzingirwa na kushambuliwa".

Anaongeza: "Tunapigania watu wa Sudan kuhakikisha maendeleo ya kidemokrasia, ambayo wamekuwa wakiyatamani kwa muda mrefu."

Chanzo: Bbc