Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amemsimamisha kazi Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ufisadi kwa shutuma za upendeleo wa kisiasa.
Wakili Busisiwe Mkhwebane anadaiwa kutawaliwa na shutuma za upendeleo wa kisiasa ambapo idadi kubwa ya uchunguzi wake toka ateuliwe mnamo 2016, umekataliwa na Mahakama, na hivyo kuzua maswali kuhusu kustahili kwake kushika wadhifa huo.
Aidha, Juni 8, 2022, Mkhwebane alisema amepokea malalamiko dhidi ya Ramaphosa ya kukiuka maadili ya kiutendaji
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Rais Ramaphosa inasema kuwa kutokuwepo kwa Wakili huyo ofisini "hakutazuia maendeleo ya uchunguzi wowote unaosubiri au unaoendelea" na kwamba atasimamishwa kazi hadi mchakato wa kumuondoa ukamilishwe na bunge.