Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan atangaza kuondoa hali ya hatari

Sudan Amani Amani Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan atangaza kuondoa hali ya hatari

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza kuondoa hali ya hatarii iliyowekwa tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021.

Taarifa ya Baraza la Utawala la Sudan linaloongozwa na jeshi imesema, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan jana Jumapili alitoa amri ya kuondoa hali ya hatari nchi nzima.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, agizo hilo limetolewa ili kutayarisha mazingira ya mazungumzo yenye matunda na yenye maana ambayo yatapelekea kufikiwa utulivu katika kipindi cha mpito.

Uamuzi huo umetangazwa baada ya mkutano na maafisa wa kijeshi kupendekeza hali ya hatari iondolewe na watu waliozuiliwa chini ya sheria ya dharura waachiliwe mara moja.

Pia hatua hiyo imechukuliwa baada ya wito wa hivi karibuni uliotolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Volker Perthes wa kuondoa hali ya hatari kufuatia mauaji ya waandamanaji wawili wakati wa maandamano ya siku ya Jumamosi yanayopinga mapinduzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live