Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu jeshi la Sudan azuia akaunti za benki za mpinzani wake

Mkuu Wa Jeshi La Sudan Azuia Akaunti Za Benki Za Mpinzani Wake Mkuu wa jeshi la Sudan azuia akaunti za benki za mpinzani wake

Mon, 15 May 2023 Chanzo: Bbc

Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametoa agizo la kufungia akaunti za benki za kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na kampuni zake tanzu.

Katika amri siku ya Jumapili, Jenerali Burhan pia alistaafisha maafisa wanne wa kijeshi wanaohusishwa na kundi hilo.

Mmoja wa maafisa walioathiriwa ni Brig Jenerali Omar Hamdan Ahmed, kamanda wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, na ambaye kwa sasa anaongoza ujumbe wa jeshi la wanamgambo kwa mazungumzo ya amani na jeshi la Sudan huko Jeddah, Saudi Arabia.

Jenerali Burhan pia alimfuta kazi gavana wa benki kuu Hussain Yahia Jankol na kumteua Borai El Siddiq badala yake.

Hakutoa sababu ya kufutwa kazi kwa Bw Jankol.

Wakati huo huo, chaneli ya serikali ya Sudan TV ilianza tena matangazo yake ya satelaiti siku ya Jumapili, wiki moja baada ya kwenda hewani.

Usambazaji wa kituo hicho umeathirika mara kadhaa tangu mapigano kati ya jeshi na RSF kuanza tarehe 15 Aprili.

Chanzo: Bbc