Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano wa amani AU waendelea Addis Ababa

Afrika Baraza Amani Mkutano wa amani AU waendelea Addis Ababa

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabaraza ya Amani na Usalama ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (AU) tangu jana Alhamisi yamekuwa yakijadili suala la kufadhili oparesheni za kulinda amani zinazoendeshwa na Taasisi ya Pan African Organiation barani Afrika.

Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika AU (PSC) jana na leo zinashiriki mkutano katika makao makuu wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Akifungua mkutano huo, Bankole Adeoye Kamishna wa Baraza la Amani na Usalama la AU amewatolea wito washiriki kuyapatia ufumbuzi masuala muhimu ya ufadhili unaotabirika, wa kutosha na endelevu kwa ajili ya shughuli za ulinzi za amani barani Afrika. Amesema suala hili limekuwa likijadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa muongo mmoja sasa. Bankole Adeoye

Nchi za Kiafrika zinaziomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchangia michango ya lazima bila ya ucheleweshaji katika uwanja huo.

Itakumbukwa kuwa Umoja wa Afrika umekuwa ukihangaika ili kufadhili oparesheni za kudumisha amani ambazo aghalabu yazo zinategemea ufadhili wa washirika kama Umoja wa Ulaya.

Parfait Onanga Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza matumaini yake kwamba majadiliano ya Addis Ababa yatapelekea kupatikana ufumbuzi ambao utawawezesha kuachana na makubaliano ya sasa ya dharula juu ya ufadhili wa shughuli muhimu za amani barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live