Mawaziri na wajumbe kutoka zaidi ya nchi 85 na mashirika ya kimataifa wanakutana mjini Accra nchini Ghana ili kubainisha dhamira yao ya pamoja kwa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.
Wanashiriki wa mkutano huo wa mwaka 2023 wa siku mbili uliong’oa nanga jana katika ngazi ya Mawaziri kutoka nchi wachangiaji wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.
Mkutano huo unalenga kupata uungwaji mkono muhimu wa kisiasa na ahadi madhubuti za kuimarisha juhudi za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa ili kukidhi changamoto na mahitaji ya sasa na ya siku zijazo, kulingana na mageuzi yanayoendelea chini ya mfumo wa Action for Peacekeeping au hatua kwa ajili ya ulinzi wa amani A4P, na mpango wa utekelezaji wa A4P+.
Operesheni maalum za kulinda amani za Umoja wa Mataifa na za kisiasa barani Afrika zimekuwa zikikabiliana na changamoto kubwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na ombi la kujiondoa kwa mpango wa Umoja wa Matagfa wa kulinda amani nchini Mali MINUSMA lililotolewa na serikali ya kijeshi ya na kufutwa kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia yta Congo MONUSCO, ambao rais wa DRC alisema mwezi Septemba mwaka huu anataka uondoke wakiwemo walinda amani wanaovalia kofia za rangi ya buluu kwa utaratibu uliopangwa kuanza kutekelezwa mapema, mwishoni mwa Desemba.
Wiki iliyopita tu, Baraza la Usalama lilikubali kusitisha ujumbe wa kisiasa nchini Sudan UNITAMS, kufuatia ombi la Serikali ya nchi hiyo la kutaka mpango huo kujiengua mara moja mwezi uliopita, ingawa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo ataendelea na juhudi za kusuluhisha mzozo mbaya wa wenyewe kwa wenyewe kati ya wanamgambo hasimunchini humo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Ghana, Shirley Ayorkor Botchwey, amezungumzia mchango wa muda mrefu wa nchi yake katika ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuwa mchangiaji wa wafanyakazi wanaovalia sare za Umoja huo askari na polisi tangu miaka ya 1960.
Pia amekiri kuhusu "rekodi ya muda mrefu na na chanya ya ulinzi wa amani barani Afrika". Amesema Ghana "Inaamini kwamba ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa una mustakabali na unasalia kuwa wa lazima na wa thamani sana katika kuendeleza amani kwenye mazingira ya migogoro duniani kote