Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano wa G7: Afrika inatafuta nafasi mpya

Mkutano Wa G7: Afrika Inatafuta Nafasi Mpya Mkutano wa G7: Afrika inatafuta nafasi mpya

Sat, 20 May 2023 Chanzo: Bbc

Afrika haitakubali kwamba "inapaswa kuendelea tu kuwa chanzo cha malighafi" kwa dunia nzima, Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Afrika ameiambia BBC.

Albert Muchanga anasema badala yake bara lake linataka mustakabali wa "mahusiano ya kweli na yenye manufaa kwa pande zote" na washirika wake wa kibiashara.

Haya yanajiri wakati mwenyekiti wa AU amealikwa kwenye mkutano wa G7 nchini Japan huku kukiwa na ushindani mkali na China kuhusu maliasili za Afrika.

Huku mataifa ya Magharibi yakitafuta uhusiano mkubwa wa kibiashara na bara hilo, kumekuwa na ziara za kutembelea nchi nyingi za Kiafrika katika maandalizi ya mkutano huo kutoka kwa viongozi wa Ufaransa na Ujerumani, pamoja na makamu wa rais wa Marekani.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alitembelea Misri, Ghana, Kenya na Msumbiji mwanzoni mwa mwezi huu akijaribu kuimarisha uungwaji mkono wa Afrika kwa juhudi zake za kukabiliana na ushawishi wa China na Urusi katika bara hilo, na pia kuhusu Taiwan na Ukraine.

Akizungumza mjini Maputo tarehe 4 Mei alisema: "Nchi nyingi za kile kinachoitwa ‘Global South’ zimeumia na kuteseka kutokana na bei ya juu ya chakula na nishati. Sababu ya suala hili inapaswa kufuatiliwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine."

Bw Muchanga anakaribisha kutambuliwa kwa matatizo ya Afrika. Anasema msukosuko uliosababishwa na janga la Covid pia inafaa kulaumiwa kwa matatizo ambayo ni "ya pande nyingi".

"Ni utambuzi wa kwamba Kaskazini na Kusini zinataka kutegemeana zaidi, na hilo linakaribishwa."

Afisa huyo wa Zambia anasema kuwa kwa sasa zama za ukoloni zimepitwa na wakati, na Afŕika inataka kupata faida zaidi kutokana na uhusiano huo kwa kujipatia ujuzi wa kuendelea zaidi thamani ya kiuchumi kutokana na maliasili yake kubwa.

"Hatutaendelea kama vyanzo vya kihistoria vya malighafi. Hilo halitawezekana kwa sababu ya ongezeko la watu, ambalo linatafuta fursa za ajira zenye staha, na hilo linaweza tu kutokana na michakato ya utengenezaji na usindikaji wa mazao ya kilimo," anasema.

"Mfano mzuri umetolewa na DRC na Zambia, watakapokuja na mradi wa pamoja wa uzalishaji wa betri za magari yanayotumia umeme." Nchi hizo mbili ndizo wauzaji wakuu nje wa shaba na kobalti zinazohitajika kwa ajili ya betri, ambazo mahitaji yake yameongezeka sana duniani kote.

Chanzo: Bbc