Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano kujadili marufuku matumizi ya plastiki kufanyika Nairobi

Plastiki Marufukuuu Nairibi Mkutano kujadili marufuku matumizi ya plastiki kufanyika Nairobi

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa nchi 175 wanakutana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, hii leo kujadili njia za kukabiliana na taka za plastiki ambazo zinaharibu mazingira katika sayari ya dunia.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa iwapoa hatua za haraka hazitachukuliwa, takriban tani milioni 11 za plastiki zinazoingia baharini kwa mwaka zitaongezeka mara tatu katika miaka ishirini ijayo.

Hii itamaanisha kati ya tani milioni 23 na 37 za plastiki zitatiririka baharini kila mwaka ifikapo mwaka 2040.

Mkutano wa Nairobi, ambao utamalizika tarehe 17 Novemba, unatazamiwa kuwaleta pamoja washiriki 2,000 wakiwmeo maafisa wa serikali na wanaharakati wa mazingira ambapo watajadili mkataba wa kukabiliana na tatizo la plastiki ambao unapaswa kutiwa saini mwakani. Mwanaharakati wa kupinga matumizi ya plastiki jijini Nairobi, Kenya

UN inasema kuwa zaidi ya tani bilioni 6.5 za platiki zinazunguka duniani na uchafuzi wa plastiki unapatikana katika kila mfumo wa ikolojia, ardhini na majini.

Inaongeza kuwa chembe ndogo ndogo za plastiki pia zimeripotiwa kupatikana katika sehemu ya miili ya wanadamu, kwenye damu, na maziwa ya mama, na hivyo kusababisha tishio kwa afya ya binadamu kutokana na viungio vya sumu katika bidhaa za plastiki.

Nchi 34 kati ya 54 barani Afrika zimepitisha sheria ya kupiga marufuku plastiki na kuitekeleza au kupitisha sheria kwa nia ya utekelezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live