Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano kuhusu Afrika ya Kati waahirishwa tena

C76be60084bed9f184f194c7ee06228e.png Mkutano kuhusu Afrika ya Kati waahirishwa tena

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUTANO wa kilele wa Kanda ya Maziwa Makuu (ICGLR) uliokuwa ufunguliwe leo mjini hapa, umehirishwa kwa mara ya pili

Umeahirishwa kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni udhibiti mji wa Bossangoa, uliofanywa na jeshi.

Jumuiya ya Kanda ya Maziwa Makuu ilitarajia kuandaa mkutano kwa lengo la kuendeleza mazungumzo, ili kumaliza ghasia zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwezi wa Desemba mwaka jana.

Wakati huo huo, Baraza la Uchumi na Jamii la Jamhuri ya Afrika ya Kati lilipokea wawakilishi wa vyama vya kiraia na vyama vya siasa vya upinzani kwa lengo la mazungumzo ya kitaifa.

Ripoti ya hitimisho la mashauriano hayo, itawasilishwa kwa mamlaka.

Chanzo: habarileo.co.tz