Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano Luanda wajadili amani DRC

Tshisekedi Amfananisha Kagame Na Adolf Hitler.jpeg Mkutano Luanda wajadili amani DRC

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mazungumzo kuhusu hali inayojiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio yaliogubika mkutano wa Luanda, hapo jana kati ya Rais Félix Thisekedi wa DRC na mwenzake wa Angola Joao Lourenco, ambae pia mpatanishi katika mgogoro huu.

Mkutano huu unafuatia mkutano mdogo ulioandaliwa Februari 18 kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia lengo ikiwa ni kuwashawishi marais wa Kongo na Rwanda kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zilizopo na kupunguza joto la uhasama unaoendelea.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete Antonio, inasemekana rais Félix Tshisekedi amekubali kimsingi kukutana na rais wa Rwanda, Paul Kagame, ikiwa sasa ni jukumu la upatanisho kufanyia kazi mkutano huo.

Idara ya mawasiliano ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia inabainisha kuwa hakuna tarehe au eneo ambalo limepangwa kwa ajili ya mkutano huo iwapo utafanyika.

Hakuna rais hata mmoja aliezungumza baada ya mkutano huo wa ana kwa ana uliodumu kwa takriban saa tatu.

Kulingana na chanzo hicho hicho, wakati wa mkutano huu mdogo, mpatanishi Lourenço alionyesha nia yake ya kupata mkutano wa moja kwa moja kati ya mkuu wa nchi wa Kongo na mwenzake wa Rwanda.

Félix Tshisekedi alikuwa ametoa sharti la kufanyika kwa mkutano kama huo kwa kuondolewa mara moja kwa wanajeshi wa RDF katika ardhi ya Kongo, kusitishwa kwa mapigano na kuwekwa katika eneo moja kwa waqsi wa kundi la kigaidi la M23

Chanzo: www.tanzaniaweb.live