Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano Jumuiya ya Madola mwakani

2fe93212bd52ab26f64b873cfcaf9a9b Mkutano Jumuiya ya Madola mwakani

Tue, 29 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUTANO wa wakuu wa serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliokuwa ufanyike Juni, mwaka huu nchini Rwanda na kuahirishwa kutokana na mlipuko wa corona, sasa utafanyika Juni 21, mwakani.

Rais Paul Kagame na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Patricia Scotland, wametangaza tarehe hiyo mpya wiki iliyopita na kwamba uamuzi huo umekubaliwa na nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

CHOGM hufanyika kila baada ya miaka miwili, ukiwa ni mkutano wa ngazi ya juu wa mashauriano na utungaji sera katika Jumuiya ya Madola na viongozi wa jumuiya hiyo waliiteua Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano unaofuata walipokutana London, Uingereza mwaka 2018.

Rais Kagame alisema mkutano huo utakaofanyika nchini humo utajadili changamoto za kiteknolojia, ikolojia, uchumi na fursa zilizopo katika nchi za jumuiya hiyo hasa vijana na jinsi ya kukabili athari za janga la corona.

Scotland alisema mkutano huo wa kihistoria kufanyika Afrika, viongozi wanatarajiwa kufikia muafaka wa masuala muhimu yanayokabili jumuiya.

“Mkutano wetu nchini Rwanda utatuwezesha kupata muafaka wa kujikita katika kukabiliana na madhara ya corona, lakini tunafahamu kuwa janga hilo halijapunguza changamoto zilizopo kama mabadiliko ya hali ya hewa, uchumi na biashara endelevu havitapatiwa ufumbuzi,” alisema.

Mkutano huo wa viongozi unatanguliwa na mikutano ya wawakilishi kutoka mitandao ya Jumuiya ya Madola ya vijana, wanawake, asasi za kiraia na biashara na utafanyika katika mji mkuu wa Rwanda wa Kigali.

Chanzo: habarileo.co.tz