Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi wa Upelelezi Kenya afungwa jela miezi minne

DCI KENYA Mkurugenzi wa Upelelezi Kenya afungwa miezi minne jela

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa idara DCI nchini Kenya George Kinoti amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kukosa kutii agizo la mahakama lililomtaka kuachilia bunduki za mfanyabiashara Jimi Wanjigi.

Kinoti anatakiwa kujisalimisha gerezani ndani ya siku saba la sivyo Inspekta mkuu wa Polisi ataingia kutekeleza hati ya kumkamata.

Jaji wa Mahakama ya Kuu Anthony Mrima mnamo Januari 2019 aliamuru DCI, Inspekta mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa mashtaka ya umma kurejesha bunduki na risasi zote zilizochukuliwa kutoka kwa makazi ya Wanjigi mnamo 2017.

Silaha zinazotafutwa ni bastola moja ya ya Smith and Wesson, bastola moja ya Glock, bunduki moja kati ya zingine.

Mrima katika kutoa agizo hilo alisema Serikali ilikosea kuchukua bunduki za Wanjigi ilhali bado ana leseni halali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live