Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi UN atua Msumbuji sakata la wakimbizi wa Jihadi

Msumbiji Un Mkurugenzi.png Mkurugenzi UN atua Msumbuji sakata la wakimbizi wa Jihadi

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, ametoa tahadhari mpya kuhusu watu laki 7 na elfu 80 waliokimbia makazi yao nchini Msumbiji, wengi wao kutokana na uasi wa miaka saba wa kundi la wanajihadi wa kiislamu wa Al Shaabab kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa hapo jana na kamishena mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi, Filippo Grandi wakati akitembelea jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Cabo Delgado, ambako wanajihadi wamesababsha mamilioni ya raia kukimbia.

Hata hivyo umoja wa mataifa umesema Takriban watu laki 6 wamerejea nyumbani, ambapo nyumba, masoko, makanisa, shule na vituo vya afya vimeharibiwa.

Ziara ya Grandi inakuja huku kukiwa na ongezeko la mashambulio mapya yaliyotekelezwa na kundi la kigaidi la Islamic State of Mozambique huko Cabo Delgado tangu Januari, baada ya kipindi cha utulivu mwaka 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live