Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkosoaji wa Rais Kagame ahukumiwa miaka 15 jela

Jela 15 Ih Mkosoaji wa Rais Kagame ahukumiwa miaka 15 jela

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkosoaji wa Utawala wa Rais Paul Kagame aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na video zake kupitia YouTube amehukumiwa miaka 15 jela Mjini Kigali.

Yvonne Idamange (42) amekutwa na makosa sita ikiwa ni pamoja na uchochezi wa ghasia na uasi, kupuuza kumbukumbu za mauaji ya kimbari, kueneza habari za uzushi na kuchochea vurugu.

Kupitia YouTube, Idamange alimshtumu Rais Kagame na Serikali yake kwa kuanzisha udikteta, kutumia mauaji ya kimbari ya 1994 kwa maslahi yao bila kuwapa msaada wowote wahanga na kugeuza eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo kuwa kivutio cha Utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live