Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkosoaji mkuu wa serikali Rwanda akutwa na hatia ya Ugaidi

Hatianijjj Paul Rusesabagina, mkosoaji mkuu wa serikali

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu ambaye alioneshwa katika filamu ya ''Hotel Rwanda'' kama shujaa aliyeokoa maisha ya watu wengi wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda amepatikana na hatia ya ugaidi katika mahakama nchini Rwanda.

Paul Rusesabagina alipatikana na hatia ya kulifadhili kundi moja la waasi akiwa mafichoni ambalo liliwauawa raia katika shambulio la 2018.

Familia yake imedai kwamba alichukuliwa na kupelekwa nchini Rwanda kwa nguvu huku wakisema kuwa ndugu yao hakushtakiwa na Mahakama huru.

Paul, amewahi kutajwa kwa sifa nyingi nzuri na zenye kuvutia katika jamii, kitu ambacho kilizima ghafla mara tu baada ya kuanza kuikosoa sana serikali ya nchini humo.

Aidha itakumbukwa kuwa, siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini humo lilifanya kikao na Jeshi la Polisi la Tanzania, kujadili njia za kukabiliana na matukio ya ugaidi ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa wote wa makosa hayo.

Hatua hii, inatajwa kama moja ya mafanikio katika kupambana na majanga ya ugaidi, huku ikikosolewa vikali na watetezi wa kisiasa nchini humo na duniani kote kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live