Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkosoaji Mkuu wa Serikali Kuhukumiwa Leo

Rusesabagina 2?fit=600%2C409&ssl=1 Mkosoaji Mkuu wa Serikali Kuhukumiwa Leo

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

BAADA ya kukaa nyuma ya nondo kwa zaidi ya mwaka mmoja, hatimaye mkosoaji mkuu wa Serikali ya Paul Kagame wa Rwanda, Paul Rusesabagina anatarajiwa kuhukumiwa leo Jumatatu, Septemba 20, 2021.

Rusesabagina (67) ambaye amekuwa mmiliki wa Hoteli maarufu nchini humo, Rwanda Hotel anatajwa kuwa aliwasaidia watu zaidi ya 1200 katika mauaji ya Kimbari ambapo alikuja kupata umaarufu mkubwa Rwanda na Marekani baada ya video yake kuonyeshwa nchini Marekani mwaka 2004.



Mfanyabiashara huyo na mkosoaji wa Serikali ya Kagame anashitakiwa kwa makosa ya ugaidi ambapo kesi hiyo wamejumuishwa wenzake 20 katika makosa hayo ya ugaidi wakihusishwa na mashambulio yaliyofanywa na kundi la waasi la MRCD- FLN dhidi ya Rwanda miaka ya 2018 na 2019, pia anakabiliwa na kosa la kufadhiri kundi la ugaidi.



Waendesha mashtaka wa Serikali waliomba hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Paul Rusesabagina aliyejitoa katika kesi hiyo mara tu ilipoanza kusikilizwa kwa madai kuwa hawezi kupata haki katika mahakama za Rwanda. Hukumu hiyo ilipaswa kutolewa mwaka jana lakini iliahirishwa bila kutolewa sababu na kupangwa kutolewa leo katika Makama Kuu ya Rwanda na iwapo atakutwa na hatia anaweza kufungwa jela miaka 25.
Chanzo: globalpublishers.co.tz