Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkewe Bob Collymore aadhimisha miaka 3 baada ya kifo chake

0fgjhs14hkii92ctho Mkewe Bob Collymore aadhimisha miaka 3 baada ya kifo chake

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mkewe mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom Bob Collymore Wambui Kabiru ameadhimisha miaka mitatu tangu kifo cakeCollymore aliaga dunia Julai, Mosi 2019 na kisha mwili wake kuchomwa katika rafadha ya Kariokor hapa jijini Nairobi kama alivyotakaWambui alisema anamkosa sana Collymore lakini yalikuwa mapenzi ya Mungu kuchukua uhai wake Wakenya pia mitandaoni wamemkumbuka kiongozi huyoMjane wa aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya safaricom Wambui Kamiru amemkumbuka mumewe miaka mitatu baada ya kifo chake.

Kamiru alisema anamkosa sana mumewe lakini ilikuwa mapenzi ya Mola kumuondoa ulimwenguni.

Shirika la Safaricom pia lilimkumbuka Collymore na kumtaja kama kiongozi ambaye hatasaulika milele kwa ajili ya utendakazi wake.

Wambui alipachika emoji za maombi kwenye ukurasa wake wa Instargram akiashiria jinsi anavyomkosa mumewe.

Collymore aliaga dunia Julai, Mosi 2019 na kisha mwili wake kuchomwa katika rafadha ya Kariokor hapa jijini nairobi kama alivyotaka.

Marehemu alikuwa akiugua ugonjwa wa saratani ambao ulimhangaisha kwa miaka kadhaa, aliwahi safiri kwenda enda Uingereza kutafuta matibabu.

Mwaka wa 2017, Collymore alipelekwa nchini Uingereza kwa matibabu zaidi na kulazwa kwa miezi tisa kabla ya kurejea nchini Juni 2018.

Bob alijiunga na kampuni ya Safaricom Novemba 2010, na kutwaa nafasi yake Michael Joseph kama Afisa Mkuu Mtendaji.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke