Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya avunja rekodi ya dunia

Dbd0194fb68ecb2eb95f239971d3e4ae Mkenya avunja rekodi ya dunia

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKENYA, Peres Jepchirchir, ameweka rekodi mpya ya dunia ya mbio za nusu marathoni kwa wanawake.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alitimua mbio kwa muda wa saa 1:05.34 huko Prague na kupunguza sekunde kutoka katika muda wa rekodi ya zamani ya dunia iliyokuwa ikishikiliwa na Muethiopia, Netsanet Gudeta, aliyoiweka mwaka 2018.

Jepchirchir alianza kuongoza katika kilometa 10 na kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.

"Nilikuwa nafikiria labda ningeweza kukimbia mbio hizo kwa kutumia saa 1:04:50, lakini nimefurahia sana," alisema bingwa huyo wa dunia wa nusu marathoni wa mwaka 2016.

Aidha, mwanariadha wa Uingereza Mo Farah naye Ijumaa alifanikiwa kuvunja rekodi ya Muethiopia mwingine ya mbio za meta 5,000 katika mbio za Diamond League huko Brussels, Ubelgiji.

Farah alikimbia mbio hiyo kwa muda wa dakika 21,330 akivunja rekodi ya dunia ya dakika 21,285 iliyowekwa na Muethiopia Haile Gebrselassie mwaka 2007.

Hiyo ni rekodi ya kwanza ya dunia kwa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 37 kushinda katika mbio za nje.

"Nilifikiri kuwa itakuwa kazi rahisi kuvunja rekodi ya dunia, lakini haikuwa hivyo kwa kweli ilikuwa ngumu sana. Rekodi imedumu kwa muda mrefu sana, “alisema Farah.

"Nimefurahi sana. Ilikuwa inafurahisha sana kurejea tena katika mbio za uwanjani. Hii ni mara ya kwanza kurejea katika mbio hii.”

Mkenya Jepchirchir alianza mbio hizo kwa kasi na kuwatoka wapinzani wake dakika 20, huku akimaliza kilometa 10 akiwa ametumia dakika 30:32.

“Namshukuru Mungu … Nimefurahi sana … nimeridhika na matokeo ingawa ningeweza kukimbia 64:50, lakini namshukuru Mungu kwa kile alichonipatia, “alisema mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26 alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mbio.

Chanzo: habarileo.co.tz