Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya anayeshukiwa kwa kutupa mtoto baharini akamatwa

Mkenya Anayeshukiwa Kwa Kutupa Mtoto Baharini Akamatwa Mkenya anayeshukiwa kwa kutupa mtoto baharini akamatwae

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanamke anayedaiwa kumtupa mtoto wake wa miezi minane kwenye bahari ya Hindi siku ya Jumapili.

Walioshuhudia waliambia vyombo vya habari kuwa mwanamke huyo alidaiwa kumtupa mtoto huyo baharini kutoka kwa feri ilipokuwa ikitia nanga katika mji wa pwani wa Mombasa.

Video ya wapiga mbizi wakimuokoa mtoto huyo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, na kuwafanya Wakenya wengi kueleza hasira zao dhidi ya mwanamke huyo na kufariji usalama wa mtoto huyo.

"[Alikimbizwa] kupata huduma ya kwanza katika Kituo cha Msalaba Mwekundu, kutibiwa na kuachiliwa akiwa katika hali nzuri na mamake akapelekwa katika kituo cha polisi kuhojiwa," K24 na Citizen TV zote zimeripoti, zikinukuu ripoti ya polisi kuhusu tukio hilo.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya awali lilisema kuwa mtoto huyo alikuwa salama katika kituo chake cha uokoaji.

Bado haijabainika ni mashtaka gani, ikiwa yapo, yatafunguliwa dhidi ya mwanamke huyo.

Chanzo: Bbc